Hatma ya Rigathi kujulikana kesho

KENYA : MAHAKAMA Kuu nchini Kenya imepanga kutoa maamuzi yake hapo kesho kuhusu bunge la seneti nchini Kenya kuendelea na hoja ya kumuondoa madarakani Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua au la.

Katika kikao hicho, Naibu Rais Gachagua anatarajia kujitetea mbele ya kikao cha wabunge na kujibu mashtaka 11 yanayomkabili yaliyoidhinishwa na wabunge 282.

Huku Jaji Mkuu Martha Koome akiteua jopo la majaji watatu watakaosikiliza hoja hizo ambapo baadaye wataweza kutoa maamuzi.

Advertisement

Hatahivyo , Naibu Rais Gachagua ameendelea kusisitiza kuwa mashtaka hayo dhidi yake yamechochewa na masuala ya kisiasa na ameonyesha kuwa na imani na Mahakama na itaweza kutoa maamuzi sahihi kuhusu kesi yake.

Nao Wakili wa upande wa utetezi wamesema mchakato huo wa kutaka kumtoa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua haukufuata misingi ya kikatiba.

SOMA:  Majaji Kenya kusikiliza kesi ya Gachagua