Hatua zaanza kupunguza ajali za vifo Afrika

UMOJA wa Mataifa (UN) umetoa taarifa ya ajali za barabarani ambapo vifo vya vijana wa Bara la Afrika vimeongezeka. Imeelezwa serikali katika bara hilo zimeazimia kuchukua hatua stahiki kukabiliana na tatizo hilo.

Taarifa ya UN imejiri ikiwa ni katika Wiki ya Kimataifa ya Usalama Barabarani, inayoadhimishwa kuanzia tarehe 15 hadi 21 Mei, taarifa hiyo imelenga kutoa msukumo wa kuchukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na ajali mbili za basi nchini Senegal ambazo ziliua watu 62 mwezi Januari.

Takwimu mbaya za ajali za barabarani zinazoongezeka hii ikiwa ni pamoja na ajali mbili za basi nchini Senegal ambazo zilipelekea watu 62 kupoteza maisha mwezi Januari.

Takwimu hizo zimeonesha Taifa la Côte d’Ivoire, idadi ya kila siku ya vifo vya ajali za barabarani imeongezeka kwa wastani wa hadi watu 46, kutoka 12 mwaka 2012.

Kiwango cha vifo vya ajali barabarani kwa mwaka huko Afrika kusini ni watu 27 kwa kila watu 100,000 na hivyo kuifanya kanda hiyo kuwa iliyoathirika zaidi na ajali za barabarani duniani.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Ulimwenguni WHO, kila mwaka, watu milioni 1.3 kote duniani hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani, na mamilioni ya wengine hujeruhiwa.

Barani Afrika, vifo vya barabarani vinachangia takriban robo ya idadi ya waathiriwa wote wa ajali hizo duniani, ingawa bara hilo lina takriban asilimia 2 ya magari yote duniani.

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani, Jean Todt, ambaye amerejea hivi karibuni kutoka kutembelea mitaa na barabara kuu za Afrika Magharibi amesema Afrika imeathiriwa zaidi na ajali za barabarani ambazo ndio chanzo kikuu cha vifo vya vijana.

Umoja wa Mataifa unasema juhudi pia zinafanywa kuwalinda watumiaji barabara walio hatarini zaidi, ambao ni watembea kwa miguu na waendesha baiskeli, ambao mara nyingi pia ndio maskini zaidi na wenye umri mdogo zaidi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x