Hatujapokea ofa Yanga, njooni mezani

TANGA: Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union, Abdallah Unenge amezima tetezi za mlinda lango wao Ley Matampi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga mwenyekiti huyo amesema hakuna ukweli juu ya tetesi hizo na bado Matampi ana mkataba wa mwaka mmoja.

“Hizo taarifa za kuhusu golikipa wetu zinatajwa tu huko nje na sisi tunazisikia wala hazijawasilishwa rasmi mpaka sasa hakuna klabu yeyote iliyokuja kimazungumzo juu ya kipa wetu  lakini ikitokea watu wamekuja tupo tayari kuzungumza kwasababu naye amebakiza mwaka mmoja”

Advertisement

Wakati huo huo amesema kuwa  wapo wachezaji ambao Coastal imewaona ndani na nje ya mipaka ya  Tanzania kiasi kwamba ikitokea yeyote akaondoka bado hakuna kitakachoharibika ndani ya klabu hiyo.