‘Hausiboi’ aua mke wa Mwenyekiti wa Mtaa

JESHI la Polisi mkoani Kagera, linamtafuta Paschale Kagwa, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22, akidaiwa kufanya mauji ya mke wa Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC Rwamishenye, Manispaa ya Bukoba.


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale, amesema kijana huyo, ambaye alikuwa msaidizi wa kazi za nyumbani kwa Mwenyekiti wa Mtaa NHC Rwamishenye, David Domick, tangu Novemba, 2022, anatuhumiwa kumuua Khadija Ismail (29) kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani jana Jumatatu Februari 13, 2023.

Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi, amesema hakuna anayejua taarifa za kijana huyo, wala eneo la asili alikotoka na kutoa wito kwa wananchi kuacha kuajiri watu ambao hawana historia nao.

Mkuu wa Wilaya ya Bukob,a Erasto Siima amefika katika familia ya Mwenyekiti huyo wa Mtaa na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano watakapokuwa na taarifa zitakazosaodia kukamatwa mtuhumiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button