LEBANON : JESHI la Israel limeshambulia maeneo ya kundi la Hezbollah kusini mwa Lebanon, katika bonde la mashariki la Bekaa na eneo la kaskazini karibu na Syria.
Msemaji wa jeshi la Israeli Daniel Hagari amesema watafanya kila kinachohitajika ili kuwarejesha kwenye makaazi yao raia wa kaskazini mwa Israel waliohamishwa.
SOMA :Israel yashambulia Lebanon
Hatahivyo Jeshi la Israel limewataka raia wa kusini mwa Lebanon kuondoka karibu na maeneo yanayotumiwa na Hezbollah ambayo wanayatumia kurusha makombora yao.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz amemshutumu kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah kuwatumia raia wa Lebanon kuhifadhi silaha na makombora kwenye nyumba zao.