Hospitali yalia Upungufu damu salama
HOSPITALI ya rufaa ya Bombo iliyopo mkoani Tanga inakabiliwa na uhitaji wa damu salama zaidi ya chupa 600 kwa mwezi huku uwezo uliopo ni kukusanya chupa 250 hadi 300 pekee.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa idara ya maabara ya damu katika hospitali hiyo , Sinde Ntobu wakati wa zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiari lililofanywa na Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga.
Amesema kuwa uhitaji wa damu kwa wagonjwa ni mkubwa katika hospitali hiyo na kuiomba jamii kuona umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari Ili kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wenye uhitaji na huduma hiyo.
“Tunaomba jamii ijitolee damu Kwa hiari kwani kwa Sasa muitikio ni mdogo Kwa wananchi kuchangia Kwa hiari hivyo amezitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Taasisi ya Bilal waliouonyesha”amesema Ntobu.
Hata hivyo Mkuu wa shule ya wasichana katika taasisi ya Bilal Sheikh Sajad Hassan amesema kuwa uchangiaji wa damu katika hospitali huwa wanajitolea kila mwaka ikiwa ni ishara ya kuonesha moyo wa kujitolea wahitaji mbalimbali hususani watoto na mama wajawazito waliopo hospitali wanaohitaji kuongezewa damu.
“Lengo la kuja kuchangia damu hapa tunaifungamanisha sadaka yetu na tukio la kuuwawa kwa mjukuu Mtume (S.A. W) Hussein Bin Allyy aliyeuwawa mwaka 61 Hijiria huko Irak aliyekuwa wakiipigania dini kwa lengo la kukemea mabaya na kuamrisha mema, aliyetoka kutetea wanyonge na wale waliodhurumiwa”