Hospitali za rufaa mikoa kutumia Tehama

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amezitaka hospitali zote za rufaa za mikoa kuanza kutumia mifumo ya Tehama ili kuboresha utoaji wa huduma.

Ummy amesema hayo leo Machi 14, 2024 wakati wa majumuisho ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi chini ya Mwenyekiti , Stanslaus Nyongo iliyotembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekotoure) na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.

Advertisement

“Katika hospitali hii ya Bugando hakuna mtu anaebeba karatasi, kuanzia mteja anaingia kumuona daktari hadi anatoka, tunataka hospitali nyingine ziige ziweze kutumia mifumo ya Tehama ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, tunataka mteja akija asikae zaidi ya masaa Matatu,”amesema Ummy.

Waziri Ummy amesema serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kutambua na kuthamini michango ya taasisi za dini katika utoaji wa huduma za afya kwa watu wa Kanda ya Ziwa ikiwemo Hospitai ya Bugando.

Amesema mbali na jitihada za serikali katika kuongeza watumishi wa wa afya, halmashauri, hospitali ziajiri watumishi wa mikataba ili kupunguza changamoto ya watumishi na kuongea kasi ya upatikanaji wa huduma za Afya nchini.