Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Liberata Mulamula katika Tafrija ya Mtandaoni ya Maadhimisho ya Miaka 73 ya Kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China
KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 73 YA KUANZISHWA KWA JAMHURI YA WATU WA CHINA
Mheshimiwa, Wapendwa marafiki Watanzania, Mabibi na Mabwana, Nina furaha kubwa kujumuika nanyi leo kusherehekea miaka 73 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kwa niaba ya Serikali ya Jamhu- ri ya Muungano wa Tanzania na kwa niaba yangu binafsi, napenda kuwapongeza kwa mafanikio haya makubwa.
Katika miaka 73 iliyopita, watu wa China chini ya uongozi bora wa Chama cha Kikomunisti cha China wamepata ustawi na ukuaji wa uchumi ambao sote tumeshuhudia na kuupenda. Inavutia kwamba zaidi ya watu milioni 700 nchini China wameon- dokana na umaskini, na hivyo kuchangia zaidi ya asilimia 70 ya kupunguza umaskini duniani kote.
Hakika haya ndiyo mafanikio makubwa zaidi ya kupunguza umaskini katika historia ya binadamu.
Kwa kuongozwa na kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani, China imeimarisha urafiki na ushirikiano kati yake na nchi nyingine ikiwemo Tanzania, na imetoa mchango muhimu katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa wanadamu na kuendeleza mambo adhimu ya amani na maendeleo ya binadamu. Mabibi na Mabwana, marafiki wapendwa wa Tanzania, tunapoadhimisha miaka 73 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, pia tunaadhimisha miaka 58 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi zetu mbili.
Tanzania na China ni marafiki wa nyakati zote, wanafurahia ushirikiano wa kina na wa pamoja.
Tanzania inazingatia kwa dhati Kanuni ya China Moja. Viongozi wetu wawili, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Xi Jinping, Rais wa Jamhu- ri ya Watu wa China, walifikia makubaliano, ambayo ni kuungani- sha Mpango wa Ukanda wa Njia (BRI) na Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na mikakati ya maendeleo ya Tanzania.
Katika suala hili, walikubaliana kupanua ushirikiano katika kilimo, usafiri, mawasiliano, utalii na nishati, ili kuimarisha maudhui ya ushirikiano wa pande zote wa Tanzania na China. Katika mwaka uliopita, tumeshuhudia ushiriki wetu katika kudumisha kasi na kufikia kilele hiki cha kimkakati cha uhusiano wetu wa nchi mbili kwa kusaidiana katika masuala yanayohusu masilahi husika na kuimarisha mabadilisha- no baina ya nchi hizo. Mabibi na mabwana, Tanzania imejitolea kuimarisha zaidi mkakati wetu wa mawasiliano na ushirikiano wa kisera, na kutekeleza kikamilifu Mipango Tisa ya FOCAC.
Tuko tayari kufanya kazi na China ili kuendeleza ari ya reli ya Tanzania-Zambia (Tazara), kuifanya kuwa ya kisasa kulingana na mwenendo wa nyakati na kuifanya Tazara kuwa njia muhimu wa usafirishaji katika ukanda huo. Pia, Tanzania iko tayari kufanya kazi na China ili kuendeleza kikamilifu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Kimataifa na Mpango wa Usalama wa Kimataifa ili kuimarisha ushirikiano wa pande zote.
Mabibi na mabwana, marafiki wapendwa, Ninapohitimisha, nichukue fursa hii kwa niaba ya Serikali na wanan- chi wa Tanzania pamoja na Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi, kufikisha salamu za kheri kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kinapojiandaa kufanya Kongamano la Kitaifa la 20 la CPC. Tunalitakia Kongamano mafanikio madhubuti. Naitakia serikali na watu wa China wafurahie maadhimisho ya miaka 73 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.
Ninawashukuru kwa umakini wenu mzuri. Asanteni Sana.