‘Huduma uchukuzi zimeimarishwa kukidhi viwango’

DODOMA: WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema wizara hiyo kupitia Mamlaka za Udhibiti nchini, zimeendelea kuimarisha na kuboresha huduma za uchukuzi ili kukidhi viwango vinavyohitajika kote duniani.

Prof Mbarawa ameeleza hayo wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 leo Mei 15, 2025 bungeni jijini Dodoma.

SOMA ZAIDI: Ujenzi viwanja vya ndege umeleta historia

Akizungumza Prof Mbarawa amezitaja mamlaka hizo zenye kusimamia huduma za uchukuzi kuwa ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCA).

Prof Mbarawa amebainisha kuwa Latra inatekeleza majukumu yake katika  kusimamia huduma za usafiri ardhini ikiwa ni usafiri wa reli na barabara, akibainisha kuwa kwa sasa wizara ipo katika hatua za mwisho katika maandalizi ya mpango wa udhibiti wa awali wa usafiri wa waya.

SOMA ZAIDI: Mbarawa ataka kasi ujenzi uwanja wa ndege Msalato

Ameeleza kuwa mamlaka ya usafiri wa angani pia inatoa huduma za udhibiti wa usafiri wa anga, viwanja vya ndege pamoja na kutoa huduma za uongozaji wa ndege katika viwanja 15 nchini pamoja na udhibiti wa anga la juu nchini Burundi, jukumu ambalo limekasimiwa kwa Tanzania na Shirika la Anga Duniani.

Pia prof Mbarawa amesema kuanzia Julai 2024 mpaka Machi 2025 Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA zimeendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi zenye kukidhi viwango vinavyohitajika.

Prof Makame ameeleza majukumu yaliyotekelezwa na TASAC kuwa ni pamoja na uchukuzi na usalama wa vyombo vya usafiri wa majini kwa Tanzania bara, udhibiti wa huduma za bandari nchini pamoja na kutoa huduma za biashara ya meli kwa bidhaa mahususi sambambana udhibiti wa uchafuzi wa mazingira unaotokana na usafiri wa majini.

Aidha, Prof Makame Mbarawa amebainisha kwamba TMA imeendelea kujiimarisha katika utoaji wa huduma kwa viwango vya Kimataifa ikitoa huduma za utabiri wa kila siku, siku kumi na utabiri wa muda mrefu sambamba na utoaji wa huduma za hali ya hewa pamoja na udhibiti na utoaji wa shughuli za hali ya hewa nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button