Human rights yailaumu Israel kusitisha huduma ya maji Gaza

GAZA, PALESTINA : SHIRIKA la Human Rights Watch limeilaumu Israel kwa kuzuia usambazaji wa maji katika Ukanda wa Gaza, hatua inayodaiwa kusababisha vifo vya maelfu ya Wapalestina, wakiwemo watoto na wazee, kutokana na utapiamlo, upungufu wa maji mwilini, na magonjwa.

Ripoti hiyo inasema kuwa Israel imekata maji, umeme, kuharibu miundombinu muhimu, na kuzuia misaada ya kibinadamu, hali ambayo imeleta madhara makubwa kwa raia wa Gaza.

Israel imekanusha madai hayo, ikisema kuwa lengo la mashambulizi yake ni kupambana na wapiganaji wa Hamas na sio raia wa Gaza. SOMA: Usitishaji vita Israel, Hamas bado kitendawili

Hata hivyo, Human Rights Watch i Smesema kuwa hatua za Israel zinaweza kuashiria nia ya mauaji ya kimbari, ingawa inasisitiza kuwa kuthibitisha nia hiyo kunahitaji ushahidi zaidi kulingana na sheria za kimataifa.

Israel, kwa upande wake, inasisitiza kuwa Hamas ndiyo inayohusika na uharibifu wa miundombinu kwa kutumia shule, hospitali, na maeneo ya makazi kama sehemu za kufanyia operesheni zake.

 

Habari Zifananazo

Back to top button