Huna tena sababu ya kunywa dawa za maumivu

KWA mara ya kwanza Afrika, teknolojia mpya ya mbadala wa dawa za maumivu imeanza kutumia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).
Hadi leo jumla ya wagonjwa 18 walipata huduma hiyo ili kuepuka maumivu ya mishipa ya fahamu, ambao huduma hiyo itaendelea kutolewa zaidi kwani takribani watu 70 huhitaji kwa siku huku kwa mwezi wakiwa 1500.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI ,Dk Respisius Boniface amesema huduma hiyo inatolewa kupitia maambara ya kisasa ya upasuaji ubongo bila kufungua fuvu la kichwa, ambapo gaharama yake ni Sh milioni moja ndani ya nchi na Sh milioni 20 nje ya nchi.
“Hii ni huduma ya kutibu maumivu ya muda mrefu utakuta mtu anakuwa na maumivu kila siku hayaishi na tumekuwa tukipata wagonjwa hao anakwambia anaumwa mgongo kila siku wakija tunawapa dawa za maumivu na kila siku anakuwa kwenye dawa sasa kutumia dawa kila siku sio vizuri,”ameeleza.
Dk Boniface amesema katika utoaji wa huduma hiyo mpya madaktari wa MOI wanashirikiana na madaktari kutoka India ili kuwajengengea uwezo wataalamu wa ndani.
Amesistiza kuwa utoaji wa huduma hiyo ni juhudi za serikali kuhakikisha huduma ambazo zinatolewa nje ya nchi zinatolewa na ndani ya nchi ikiwa katika uelekeo wa kwenda katika utalii wa matibabu.
“Ndio maana tumeanzisha hii leo unachomwa kama sindano kwa kutumia mitambo tuliyonayo katika maabara ya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu ku X-Ray za hali ya juu ambayo inamuelekeza daktari wapi pa kuweka dawa na kuchomwa kupitia mtambo.
Amesema baada ya mgonjwa kupata huduma hiyo hatapata mamumivu na ataruhusiwa kutoka hospitali siku ya pili au tatu.
“Watu walikuwa wanakwenda nje ya nchi kutafuta huduma gharama nje ya nchi Sh milioni 20 sasa hapa inapatikana kwa Sh milioni moja,”ameeleza.
Huduma hiyo ya kupunguza maumivu ya mgongo mnafanya upasuaji au ni tiba tu, mimi ni muhanga pia, na je bima inatumika kwa matibabu?