Huyu ndiye mwanzilishi wa Instagram
KEVIN Systrom ana umri wa miaka 40 ni mtayarishaji programu za kompyuta na mjasiriamali raia wa Marekani. Systrom ndiye mwanzilishi wa tovuti ya Instagram akishirikiana na Mike Krieger.
Systrom alijumuishwa kwenye orodha ya wajasiriamali matajiri zaidi wa Marekani walio chini ya umri wake. Alijiuzulu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Instagram mnamo Septemba 24, 2018.
Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Buffer’ Instagram imefikisha watumiaji bilioni 2.4, facebook ikiongoza kwa kuwa na watumiaji bilioni 3.4 mpaka kufikia Julai 2024.
Meta Platform ilinunua Instagram kwa Dola bilioni 1 mnamo 2012, pesa nyingi wakati huo kwa kampuni iliyokuwa na wafanyikazi 13. Instargram inachangia zaidi ya Dola bilioni 20 kwa mapato ya kila mwaka ya Meta Platforms.
MAREKANI: KEVIN Systrom ana umri wa miaka 40 ni mtayarishaji programu za kompyuta na mjasiriamali raia wa Marekani. Systrom ndiye mwanzilishi wa tovuti ya Instagram akishirikiana na Mike Krieger.
Systrom alijumuishwa kwenye orodha ya wajasiriamali matajiri zaidi wa Marekani… pic.twitter.com/oJnIP2Dscb
— HabariLeo (@HabariLeo) September 24, 2024
Baada ya kuhitimu Chuo Kikuu cha Utafiti cha Stanford nchini Marekani mwaka 2006, Systrom alijiunga na kampuni ya Google nakufanya kazi kwenye idara ya Google Gmail na Calendar, akiwa hapo alitumia miaka miwili na kuendelea na maisha mengine.