IAA, TPF  yasaini kushirikiana

CHUO  cha Uhasibu Arusha (IAA) na Jeshi la Polisi Tanzania (TPF) kupitia shule ya Polisi-Moshi wamezindua rasmi ushirikiano wa kitaaluma.
Uzinduzi huo umefanyika leo  Juni 9, 2023 katika chuo cha Polisi Moshi.
Akizindua rasmi ushirikiano huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camilius Wambura amesema makubaliano hayo  ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Agosti 30, 202
Katika maagizo hayo, Rais Samia alilitaka Jeshi la Polisi kuboresha mifumo yake ya utendaji kazi hasa katika kuzuia uhalifu wa mitandao.
“Hivyo, ,  ushirikiano huu wa kitaaluma unaenda kutekeleza agizo hili. ’’ Amesema Wambura.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka ameushukuru uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kuwa tayari kushirikiana na IAA hasa katika suala zima la taaluma.
Prof. Sedoyeka amesema programu  watakazoshirikiana na Jeshi la Polisi kwenye kutoa mafunzo ni pamoja na Shahada ya Sayansi katika Usalama wa Mitandao, Shahada ya Usalama wa Masomo ya Kimkakati, Shahada ya Uzamili ya Ulinzi wa Taarifa,  na Shahada ya Uzamili ya Amani na Masomo ya Ulinzi.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi IAA Dkt. Mwamini Tuli amesema Jeshi la Polisi limeonyesha nia madhubuti ya ushirikiano, hivyo kupitua elimu watakayoipata itasaidia kuboresha ulinzi na usalama,na kwa pamoja watahakikisha wanawaanda watumishi mahiri wenye weledi mkubwa.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na makamanda wa polisi, wafanyakazi wa IAA pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button