IAA yawainua vijana 8,600

ZAIDI ya vijana 8,600 wamefikiwa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kupitia programu za ujasiriamali na ubunifu, hatua iliyowezesha vijana 1,520 kubuni mawazo ya biashara na kuanzisha zaidi ya biashara 50, huku kampuni 12 zikisajiliwa rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu miradi ya maendeleo na fursa za vijana kwa mwaka 2025/2026, Mkuu wa chuo hicho Prof. Eliamani Sedoyeka amesema mafanikio hayo yanatokana na kuimarishwa kwa Kiatamizi (Incubator)/IAA Business Start Up Centre kinachowawezesha wanafunzi kugeuza mawazo yao kuwa miradi halisi ya kibiashara.

Amesema kampuni zilizoanzishwa zimejikita katika sekta za biashara, teknolojia, sanaa na uhifadhi wa mazingira, na tayari zimeanza kutoa ajira kwa wahitimu na vijana wengine, hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi. SOMA: Serikali yasaini mkataba ajira kwa vijana nje ya nchi

Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa IAA ni miongoni mwa taasisi zilizonufaika na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaolenga kuimarisha ubora wa elimu  ya juu na kuendana na mahitaji ya soko la ajira. Ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika elimu na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button