Idadi waliokufa Florida yafikia kumi

FLORIDA : WAKAAZI wa Florida wameathirika na uharibifu mkubwa wa Kimbunga Milton kilichosababisha uharibifu wa  majumba,miundombinu ya umeme maji na barabara.

Kimbunga Milton kilikuja na upepo mkali ambapo majumba mengi yalibomoka na kusababisha watu kumi kupoteza maisha,

Eneo lenye idadi kubwa ya watu la Tampa limenusurika kupigwa na kimbunga hicho ambacho kilihofiwa huenda kingekuwa na madhara makubwa sana.

Advertisement

Hata hivyo, uharibifu  mwingine umetokea katika maeneo ya jimbo  la Florida ambako paa la uwanja wa mchezo wa Baseball liling’olewa huku mifumo ya umeme ikiharibiwa na kuwaacha watu zaidi ya milioni tatu kukosa nishati ya umeme.SOMA : Kimbunga Milton chabisha hodi Florida

Kufuatia kimbunga Milton , Serikali ya Marekani imepanga kupeleka misaada ya kibinadamu.