Idadi waliohama makazi yaongezeka -IDMC

MAREKANI : IMEELEZWA kuwa Idadi ya wakazi waliohama makazi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uwepo wa mizozo, machafuko ya kisiasa na majanga katika Bara la Afrika imeongezeka  mara tatu ya  idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Ripoti ya Shirika linalofuatilia mienendo ya watu kulazimika kuyahama makazi yao ndani ya nchi zao –IDMC imesema  kufikia mwisho wa mwaka 2023 bara la Afrika lilikuwa  na watu wasiopungua milioni 35 ambao wanaishi nje ya makazi yao.

Mkuu wa shirika hilo, Alexandra Bilak amesema idadi hiyo ni karibu ya nusu ya idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao duniani kote. Soma: Uganda kupitia upya sera ya wakimbizi

Advertisement

Taarifa imefafanua kuwa majanga ya mafuriko  pekee yamesababisha  zaidi ya watu asilimia 75 kuyahama makazi yao huku wengine asilimia 11 wakihama kutokana na tatizo la ukame.