INEC yawafunda wasimamizi 86 Arusha, Manyara

ARUSHA; WASHIRIKI 86 kutoka Mikoa ya Arusha na Manyara, ambao ni waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi, maofisa uchaguzi na maofisa ununuzi wanapatiwa mafunzo jijini Arusha.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), inaratibu na kuendesha mafunzo hayo kwa watendaji hao maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

Akifungua mafuzo hayo, Dk Zakia Mohamed Abubakar, amabye ni Mjumbe wa INEC, alisema watendaji hao wamepewa dhamana ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa Tanzania Bara, ambapo ni jukumu kubwa na nyeti kwa mustakabali wa Taifa.
“Nawasisitiza kuwa mjitahidi na mjiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wa Uchaguzi, “amesema Dk Abubakari.
Amewataka watendaji hao kufanya utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema, ili kubaini mahitaji maalumu ya vituo husika na kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri, ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.

Amewasisitiza watendaji hao kuwa wasome kwa umakini katiba, sheria,kanuni ,miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na tume



