Iran yaikosoa Israel kuhusu usitishaji mapigano

TEHRAN : SERIKALI ya Iran imetangaza kutokuwa na imani na hatua ya Israel ya kutangaza usitishaji wa mapigano, ikisema bado ina shaka juu ya dhamira ya taifa hilo hasimu katika kuhitimisha mzozo uliozua maafa makubwa kati yao.

Mkuu wa majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, alinukuliwa na televisheni ya taifa akieleza kuwa Israel haionekani kuwa na nia ya kweli ya kusitisha mapigano, akisisitiza kuwa Iran iko tayari kujibu kwa nguvu endapo itashambuliwa tena.

“Tuna mashaka makubwa kuhusu utii wa Israel. Tupo tayari kuchukua hatua kali za kijeshi iwapo watarudia kushambulia,” alisema Jenerali Mousavi. SOMA: Samia aagiza Watanzania walio Iran, Israel kurudi nchini

Kauli hiyo inakuja siku sita baada ya Rais wa Marekani wa zamani, Donald Trump, kutangaza makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya mataifa hayo mawili.

Mapigano hayo yaliyochukua siku 12 yalianza baada ya Israel kushambulia maeneo ya Iran kwa mabomu, ambapo baadhi ya makamanda waandamizi wa jeshi na wanasayansi wanaoshukiwa kushiriki kwenye mpango wa nyuklia waliuawa.

Iran ilijibu mashambulizi hayo kwa kurusha makombora katika miji mbalimbali ya Israel, hali iliyochochea taharuki na uharibifu mkubwa. Hadi sasa, hali ya tahadhari bado imetanda huku jumuiya ya kimataifa ikitoa wito wa kudumishwa kwa usitishaji wa mapigano na kutafutwa kwa suluhu ya kudumu kati ya pande hizo mbili.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button