WASHINGTON DC : SERIKALI ya Marekani imeitaka Israeli kujiepusha na operesheni za kijeshi nchini Lebanon, baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kusema Lebanon inaweza kuwa kama Gaza.
Huku Mkuu wa Jeshi la Israel, Herzi Halevi, akiahidi kuendelea kupiga ngome za Hezbollah ambapo mashambulizi hayo yameua zaidi ya watu 1,200 tangu Septemba 23.
Netanyahu amewataka watu wa Lebanon kuiweka huru nchi yao kutoka kwa Hezbollah ili kuepuka vita vya muda mrefu.
SOMA : Jeshi la Israel laingia Lebanon
Rais wa Marekani, Joe Biden, alimshauri Netanyahu kuepuka kusababisha madhara kwa raia wa Lebanon, hasa katika maeneo yenye wakazi wengi kama Beirut.