LEBANON : JESHI la Israel limefanya mashambulizi ya anga yaliyolenga taasisi ya fedha inayodaiwa kuhusika kwa ufadhili wa silaha za wapiganaji wa Hezbollah wakati wakiendelea kutanua mashambulizi nchini Lebanon.
Mashambulizi ya anga ya Israel yalilenga matawi ya taasisi ya Al-Qard Al-Hassan katika miji ya Nabatiyeh na Tyre.
Hatahivyo, taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel imedai kuwa maeneo kadhaa ya taasisi hiyo yakiwemo matawi yake ya benki yalikuwa yakitumiwa na wapiganaji wa Hezbollah.
Mashambulizi haya yanaashiria kutanuka kwa vita vya Israel dhidi ya Hezbollah katika kupunguza uwezo wa kundi hilo kuendesha operesheni zake.
Taasisi hiyo inafahamika kwa kutoa mikopo nchini Lebanon ambako mifumo ya kawaida ya kibenki ilisambaratika miaka mitano iliyopita kutokana na mgogoro mbaya wa kiuchumi.
SOMA : Israel yashambulia ngome za Hezbollah