Israel yaua Wapalestina 3, wajaruhi 37

IMERIPOTIWA vikosi vya jeshi la Israel vimevamia kambi ya wakimbizi ya Jenin na kuwauwa Wapalestina watatu pamoja na kuwajeruhi 37. Al-Jazeera imeeleza.

Taarifa iliyochapishwa leo juni 19, 2023 na mtandao huo, likilinukuu shirika la habari la Wafa, likidai kuwa uvamizi huo umefanyika leo Jumatatu asubuhi, huku wanajeshi wa Israel wakivamia kambi hiyo kwa kufyatua risasi za moto, maguruneti na gesi yenye sumu.

Wizara ya Afya ya Palestina imewataja waliouawa kuwa ni Khaled Darwish, 21, Qassam Sariya, 19, na Ahmed Saqr, 15.

Jeshi la Israel lilisema kuwa uvamizi huo ulikuwa wa kuwakamata washukiwa wawili na kwamba jeshi hilo walikabiliwa na mashambulizi ambayo yalisababisha “majibizano makubwa ya risasi”.

Mmoja wa washukiwa waliokuwa wakiwafuata ni “mtoto wa kiongozi wa Hamas aliyefungwa,” Imran Khan wa Al Jazeera alisema kutoka Jerusalem Magharibi.

Wakati magari ya jeshi la Israel yalipokuwa yakitoka kambini, taarifa ya jeshi ilisema, “gari la kijeshi liligongwa na kilipuzi, na kuharibu gari”, baada ya hapo helikopta za kijeshi zilipiga risasi kuelekea upande wa watu wenye silaha na hivyo vikosi kuondoka.

Picha za video zilizothibitishwa na shirika la Sanad zilionyesha helikopta ya Israel ikirusha roketi kwenye kambi hiyo na ndege za uchunguzi zikielea juu.

Bezalel Smotrich, Waziri wa Fedha wa Israel, ametoa wito hadharani wa “operesheni kubwa katika Ukingo wa Magharibi “unaokaliwa”, akiongeza kuwa “wakati umefika kufanya maamuzi”.

Habari Zifananazo

Back to top button