Jaji Chande: Asisitiza tume iko huru
DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande, amesema tume hiyo ni huru kwa asili kuanzia sheria iliyoianzisha, viapo vya wajumbe na hakuna mtu anayewaamrisha chakufanya.
Jaji Chande alifichua Tume anayoiongoza ina watu makini, ambao wanajua jambo lililotokea Oktoba 29 ni kubwa linalohitaji weledi katika kushughulikia.
Aliongeza baada ya kupewa hadidu za rejea tume hiyo iliweka kanuni zake yenyewe akisisitiza: “Uhuru wetu ulianza baada ya kupokea hadidu za rejea. Tuliandaa kanuni zetu. Tuliamua ushihidi uwe ni hiari kwa mtu kuutoa.”



