Jaji Chande awahimiza watanzania kutoa ushahidi

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande, amewataka Watanzania kutumia muda wa nyongeza kutoa ushahidi zaidi, kwa kuwa anatambua matumaini yao makubwa na jumuiya ya kimataifa kwa tume hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam, Jaji Chande pia alitaja sababu nne za tume kuomba muda wa nyongeza, akianisha moja ni kuendelea kupokea na kuchambua ushahidi kisayansi hivyo, kuwataka Watanzania zaidi kuwa huru kujitokeza.
Katika mkutano huo, ambao alipokea maswali mbalimbali na kujibu kwa kina, Jaji Chande alisema anajua matumaini makubwa ya watu kuhusu tume na aliwahikikishia iko huru.
“Kazi ya Tume inaongozwa na ushahidi. Mtiririko wa ushahidi ni mkubwa. Ndiyo maana tumeomba muda hatuwezi kuacha ushahidi uliotufikia. Tunaamini muda tulioomba utatosha. Wengine wenye ushahidi tunawakaribisha. Sisi hatulazimishi watu kwa amri bali hiari katika kutoa ushahidi,”alifafanua Jaji Chande.



