James Comey afunguliwa mashtaka

WASHINGTON, Marekani: ALIYEKUWA mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la FBI, James Comey, ameshtakiwa kwa tuhuma za kutoa taarifa zisizo sahihi mbele ya Bunge la Marekani na kuzuia haki kutendeka.
Rais Donald Trump alimfuta kazi mnamo mwaka 2017, muda mfupi baada ya kuthibitishwa kuwa alichunguzwa kuhusiana na madai ya uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016. Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Pam Bondi, alisema hati ya mashtaka inaonyesha dhamira ya kuwawajibisha waliotumia vibaya nyadhifa zao. SOMA: Bossi FBI: Msijibu ’emails’ za Musk
Mashitaka yanahusiana na ushahidi alioutoa Comey mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu madai ya kufichua taarifa nyeti. Ikiwa atapatikana na hatia, Comey atafungwa kifungo cha miaka mitano jela kwa mujibu wa sheria za Marekani.



