Japan kushirikiana na SUA sekta ya kilimo

SERIKALI ya Japan kupitia ubalozi wake nchini Tanzania itaendelea kushirikiana vizuri na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) hasa katika sekta ya kilimo na usindikaji wa mazao ya vyakula ikiwa ni moja ya sehemu ya kilimo kinachofanyika nchini humo.

Balozi wa Japan nchini , Yashushi Misawa alisema hayo wakati wa makabidhiano ya vitabu vitabu 61 vya lugha ya Kingereza kwa Menejimeti ya Chuo Kikuu hicho kwenye Kamapsi ya Edward Moringe.

Lengo la vitabu hivyo ni kuwasaidi watafiti, wasomi na wanafunzi ili kukuza uelewa kwa wataalam na wasio wataalam katika kuchangia maendeleo ya rasilimali watu.

Misawa alisema chuo hicho ni moja ya vyuo vyenye matumaini makubwa nchini Tanzania kutokana na ushirikiano wa karibu na nchi yake ambao umendelea kudumu kwa muda mrefu.

Alisema anaamini kupitia vitabu hivyo wataenda kupata wanafunzi kutoka chuoni hapo, vilevile nchi yao inaweza kushirikiana vizuri na SUA hasa katika sekta ya kilimo na usindikaji wa vyakula kama moja ya sehemu ya kilimo ambayo hata wao wamekuwa wakiufanya.

Alisema kuwa vitabu hivyo vinahusisha mada mbalimbali ikiwemo kilimo na teknolojia, siasa, uchumi, jamii na utamaduni wa Japan lakini pia na nchi mbalimbali .

Balozi huyo alisema ni matumaini yake kuwa, vitabu hivyo vitatumika kama njia ya muingiliano baina ya wanafunzi pamoja na watafiti ili kuongeza uelewa wao.

‘‘Tumetoa Vitabu kwa Taasisi Zaidi ya 1,100 kote Ulimwenguni hadi sasa na , kwa Tanzania kwa SUA kinakuwa ni Chuo Kikuu cha nne kupatiwa vitabu baada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dodoma (UDOM) , UDOM na DUCE” alisema Balozi Misawa

“ Nikiwa kama shahidi Ubalozi wa Japan nchini Tanzania tuliamua kupendekeza SUA kama mwenyeji kwa sababu ya ushirikiano wa karibu na wa muda mrefu tulionao baina yetu’’ alisisitiza Balozi Misawa kwa lugha fasaha ya kiswahili

Naye Makamu wa Mkuu wa SUA, Profesa Raphael Chibunda alisema ziara ya balozi huyo katika ni katika kuendeleza mashirikiano baina yao ambayo yamekuwepo tangu miaka ya 70 na yamekuwa yakiendelea kuimarika siku hadi siku.

Profesa Chibunda alisema, Japan imekuwa mfadhili katika miradi mbalimbali chuoni hapo , pia kuwapatia nafasi Watafiti na Wanataaluma wao kufanya kazi pamoja na Watafiti na wanataaluma wa Kijapan.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho alisema wamekuwa wakiwapatia nafasi ya kupeleka kuwasomesha wanataaluma wao ambapo katika siku chache zijazo wanataaluma watatu wanaenda kuanza masomo yao ya Uzamivu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Japan.

“ Kwetu sisi SUA tunamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Haasan , kwa kuendelea kuimarisha uhusiano wa nchi ya Tanzania na nchi za kigeni” alisema Profesa Chibunda

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maktaba ya Taifa ya Kilimo SUA ,Profesa Wulystan Mtega alisema kuwa watumiaji wa Maktaba yao wanahitaji machapisho mbalimbali na kwamba vitabu hivyo vitawasaidia hasa katika kuelewa mbinu mbalimbali ambazo Japan wamekuwa wakizitumia hasa katika kujikwamua kiuchumi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button