Jela miaka mitatu kwa kuiba mtoto

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imemuhukumu Veronica Nyanda (32) mkazi wa mtaa wa Shunu kata ya Nyahanga kifungo cha miaka mitatu jela kwa kukiri kosa la kuiba mtoto wa miezi mitatu.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Christina Chovenye alitoa hukumu hiyo Jana huku akieleza adhabu hiyo imetokana na kosa la wizi wa mtoto kinyume cha kifungu 169( 1) (a) huku mtuhumiwa akitenda kosa hilo tarehe 21, Septemba 2023.

Chovenye alisema mtuhumiwa huyo alienda kwenye nyumba anayoishi mtoto huyo na wazazi wake katika eneo la Wame mtaa wa Mwime kata ya Zongomela ambapo alienda kwa maelezo ya mtuhumiwa kudai madeni yake maeneo hayo.

Chovenye alisema ilipofika usiku alilala na kesho yake asubuhi wazazi wa huyo mtoto walimuacha nyumbani mtuhumiwa na mtoto na wao wazazi wakaenda shambani ndipo alipopata mwanya wa kuiba mtoto huyo nakuondoka.

“Mnamo tarehe 25,Septemba 2023 mtuhumiwa alikamatwa na Jeshi la polisi akiwa nyumbani kwake eneo la Shunu akiwa na mtoto huyo na kufunguliwa kesi hii mahakamani” alisema Chovenye.

Chovenye alisema mtuhumiwa baada ya kumuhoji alidai anawatoto kumi wa kuzaa nyumbani kwake na watoto wanne walikwisha fariki hivyo anapenda kuwa na watoto hakumchukua huyo kwa lengo baya.

Chovenye alisema wakati akiendelea na kesi ya wizi wa mtoto tayari ana kesi nyingine ya wizi ya kutuhumiwa kuiba mtoto eneo la Mwakitolyo ambayo kesi hiyo inaendelea mahakamani akiwa kwenye zoezi la wizi amekuwa akitumia majina ya Veronika Alex Nyanda na Kareny Peter.

Chovenye alisema mtuhumiwa amekiri kosa mwenyewe la kuiba mtoto ndipo mahakama ikatoa adhabu hiyo.

Mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa Serikali Evodia Baimo alisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julia
Julia
1 month ago

Earn money in USA, high scores from trusted resources. Work at your own pace. Regular Payments. Search in different job categories. Work anywhere on your vs03 computer, laptop or mobile phone. Update your profile at any time.
.
.
Detail Here———->>> http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Julia
Angelhompson
Angelhompson
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by Angelhompson
MONEY
MONEY
1 month ago

UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER

R.jpeg
MONEY
MONEY
1 month ago

UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER ..

11.jpg
MONEY
MONEY
1 month ago

UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER …

Screenshot_20190909-051939.jpg
MONEY
MONEY
1 month ago

UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER ……..

Screenshot_20190809-051607.jpg
MONEY
MONEY
1 month ago

UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER /

OIP (2).jpeg
MONEY
MONEY
1 month ago

UBUNIFU – ALILIA NA KUPAMBANA KUANDIKWA/KUYAUWA MAGAZETI YA GROBAL PUBLISHER ‘

OIP (1).jpeg
Back to top button
8
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x