SUDAN: Mkuu wa Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amenusurika kufa katika jaribio la mauaji lililosababisha vifo vya watu watano.
Kwa mujibu wa Msemaji wa jeshi, Nabil Abdallah, Jenerali Burhan pamoja na makamanda wengine wako salama baada ya shambulio hilo.
Jaribio hilo lilifanyika wakati Jenerali Burhan akihudhuria sherehe ya kufuzu kwa wanajeshi kutoka vyuo vya anga na majini katika eneo la Jebit, mashariki mwa Sudan.
Hata hivyo, Msemaji wa jeshi amethibitisha kuwa vikosi vya wapiganaji wa Rapid Support Force (RSF) vinahusishwa na shambulio hilo.
Mpaka sasa, wapiganaji wa RSF hawajatoa taarifa yoyote kuhusu shambulio hilo, na hali ya kisiasa nchini Sudan inazidi kuwa tete huku viongozi wa kijeshi wakijaribu kudhibiti hali ya usalama.
SOMA: UN yataka usitishwaji mapigano Sudan