Jeneza la Malkia Elizabeth II laelekea ibada ya kifamilia

Jeneza la Malkia Elizabeth II laelekea ibada ya kifamilia

JENEZA la Malkia Elizabeth II, limeanza safari yake ya mwisho kutoka Westminster Abbey kuelekea Kasri la Windsor kwa ajili ya ibada ya kifamilia.

Misa ya kidini ya kumuaga malkia huyo imekwishafanyika katika ukumbi wa Westminster Abbey ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, aliyetoa mahubiri na kusema kuwa malkia aligusa maisha ya watu wengi katika miaka yake 70 ya utawala.

Jengo hilo la Canterbury ndio jengo alilofungia ndoa na mume wake Philip Duke, mwaka 1947 na ndipo alipovikwa taji la umalkia Juni 2, mwaka 1953.

Advertisement

Mamia ya watu mashuhuri wamehudhuria mazishi yake wakiwemo mawaziri wakuu wa zamani wa Malkia pamoja na Rais wa Marekani, Joe Biden na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.