Jeshi la Congo, Burundi wazuia M23 kuingia Bukavu

CONGO : WANAJESHI  wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wakisaidiana na jeshi la Burundi, wamefanikiwa kufanya juhudi za pamoja kuwarudisha nyuma waasi wa M23, waliokuwa wakisonga mbele mashariki mwa Congo na kuelekea mji mkuu wa Kivu Kusini, Bukavu.

Mapema wiki hii, waasi hao, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, waliteka mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma, baada ya mapigano makali na wameapa kusonga mbele hadi Kinshasa, mji mkuu wa DRC.

Hali hiyo inajiri muda mfupi baada ya viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kutoa tamko la dharura la kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mapambano yake dhidi ya M23.

Advertisement

SADC ilifanya mkutano wa dharura nchini Zimbabwe kujadili mzozo unaoendelea mashariki mwa Congo, ambao umeibua wasiwasi kuhusu usalama wa kikanda.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), watu 700 wamepoteza maisha kutokana na mapigano hayo katika kipindi cha wiki moja. SOMA: CONGO: Serikali kuimarisha usalama Goma

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *