Jeshi la Polisi kushirikiana na TIA katika tafiti na mafunzo

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura amesema Jeshi hilo limewekeza zaidi katika kufanya utafiti, elimu na mafunzo ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa jamii na kwenda na mabadiliko ya dunia ya sasa.

IGP Wambura amesema hayo wakati aliposhiriki hafla ya utiaji Saini Hati ya makubaliano na mashirikiano baina ya Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam ambapo ushirikiano huo utawezesha Jeshi hilo kujiendeleza kitaaluma hasa eneo la mafunzo na tafiti mbalimbali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo amesema kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kufaidi mashirikiano yaliyopo kati ya Chuo cha Uhasibu Tanzania huku akibainisha kuwa changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii zitapatiwa ufumbuzi kutokana na mashirikiano walioingia na Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es salaam DPA Dk. Lazaro Mambosasa amesema kuwa, mashirikiano kati ya Jeshi la Polisi kupitia Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam na na Tasisi ya uhasibu Tanzania ni ya awali ambayo yamejikita zaidi kwenye eneo la usalama na kitaaluma.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button