Jeshi la Sudan larejesha udhibiti wa Ikulu

SUDAN : JESHI la Sudan limefanikiwa kurejesha udhibiti wa majengo ya ikulu yaliyo jiji kuu la Khartoum, leo hii, baada ya kujiunga na wanamgambo wa RSF walichukua majengo hayo katika siku za mwanzo za vita, karibu miaka miwili iliyopita.
Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, msemaji wa jeshi la Sudan, Nabil Abdallah, ameeleza kuwa vikosi vya serikali vimefanikiwa kuvuruga vikosi vya RSF, na kuteketeza silaha nyingi za kivita zilizokuwa katika mikono ya wapiganaji hao.
Mapigano makali yalishuhudiwa kati ya pande hizo mbili kabla ya jeshi la Sudan kupata ushindi mkubwa, ambao ni moja ya mafanikio makubwa zaidi tangu kuanza kwa vita mwezi Aprili, 2023.
Majengo ya ikulu, yaliyopo katikati ya mji mkuu Khartoum, yamekuwa ni uwanja wa mapigano makali baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa RSF katika miezi ya hivi karibuni.
SOMA: Watu 200 wauawa katika mashambulizi ya Sudan



