Jeshi lasitisha usafirishaji nafaka

NIGER : UTAWALA wa kijeshi nchini Niger umepiga marufuku mauzo ya nje ya nchi ya nafaka kwa nchi zote isipokuwa nchi zinazoongzowa kijeshi ikiwemo Burkina Faso na Mali.
Taarifa iliyotolewa na serikali imesema kuwa kiongozi wa kijeshi wa Niger Abdourahmane Tiani amechukua hatua hiyo ili kulinda usambazaji wa soko la ndani na upatikanaji wa kutosha wa bidhaa zinazotumiwa kwa wingi.
Kiongozi huyo wa kijeshi amesema mtu yeyote atakayekiuka basi atakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya jinai.
Ingawa vikwazo hivi hapo awali vilisitishwa lakini soko la chakula nchini humo likaendelea kudorora na kusababisha mfumuko wa bei kuongezeka. SOMA: Marekani kuondoa wanajeshi Niger