MSUMBIJI : VIKOSI vya ulinzi na usalama nchini Msumbiji leo vimepiga doria katika baadhi ya mitaa ya mji wa Maputo ili kusitisha maandamano yaliyopangwa kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo yalionekana yalikumbwa na udanganyifu.
Mji wa Maputo wenye idadi ya zaidi ya watu milioni moja ulikuwa tulivu bila heka heka huku maduka, mabenki, shule na vyuo vikuu vikifungwa.
Mgombea wa upinzani nchini humo , Venancio Mondlane anaamini alishinda uchaguzi huo ndio maana aliamua kuitisha maandamano makubwa leo hii kwa lengo la kupinga matokeo ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa karibu watu 18 wameuwawa katika machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi huo huku shirika lisilo la kiserikali linalojulikana kama Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu, CDD, limesema kuwa idadi ya waliofariki imefikia 24. SOMA: Maandamano yatikisa Msumbiji