JK ateta na Rais wa Algeria

ALGERIA: RAIS Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete, amekutana na Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune kwa mazungumzo kuhusu uhusiano wa muda mrefu na wa kindugu kati ya mataifa hayo mawili.

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kushirikiana katika sekta muhimu kama biashara, uwekezaji, elimu, afya, na ulinzi.

Mkutano huo umefanyika nchini Algeria, ambapo viongozi hao wawili wamehimiza mshikamano na ushirikiano ulioasisiwa enzi za harakati za ukombozi wa Afrika. Pia wamejadili namna ya kuendeleza uhusiano huo kwa manufaa ya mataifa yote mawili.

Kikwete amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, na amewasilisha dhamira ya Tanzania ya kuimarisha ushirikiano na Algeria. Aidha, amebainisha maono ya pamoja kuhusu ukuaji wa uchumi na utulivu wa kikanda.

Kwa upande wake, Rais Tebboune amepongeza urafiki wa kihistoria kati ya Algeria na Tanzania na kusisitiza kuwa Algeria ipo tayari kuendeleza ushirikiano katika sekta mbalimbali zenye maslahi ya pamoja.

Kabla ya mkutano wao, Rais Mstaafu Kikwete alipokelewa katika Ikulu ya Algiers na Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Kitaifa ya Nje na Masuala ya Afrika, Ahmed Attaf, Waziri wa Afya, Abdelhak Saihi, pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi wa Algeria, Boualem Boualem

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button