JK avishwa nishani ya heshima

DAR ES SALAAM; Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yanafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JICC), Dar es Salaam.