JKCI yaanza tiba kupunguza msisimko shinikizo la damu

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeweka historia mpya nchini Tanzania, Afrika Mashariki na Kati baada ya kuanza kutoa matibabu mapya ya kibingwa ya kupunguza msisimko wa shinikizo la damu kwenye mishipa ya figo, ujulikanao kama Renal Denervation Therapy.

Hii ni mara ya kwanza kwa matibabu hayo kutolewa katika ukanda huu wa Afrika.

Matibabu hayo yameanza kutolewa leo katika taasisi hiyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na shinikizo la juu la damu la muda mrefu ambalo hushindikana kudhibiti kwa kutumia dawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge, amesema shinikizo la juu la damu linachangia takribani asilimia 25 ya magonjwa yasiyoambukiza, na kuwa chanzo kikubwa cha vifo vya ghafla pamoja na ongezeko la wagonjwa wanaohitaji huduma ya dialysis kutokana na figo kushindwa kufanya kazi.

“Matibabu haya yanatumia mashine ya radio frequency ultrasound ambayo huunguza mishipa ya damu inayoelekea kwenye figo ili kupunguza shinikizo la damu na kuurudisha mwili katika hali ya kawaida,” amesema Dkt. Kisenge.

Ameongeza kuwa matibabu hayo hupunguza hatari ya kiharusi, matatizo ya figo na husaidia kudhibiti homoni zinazochochea kupanda kwa shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa Dk Kisenge, huduma hiyo ni ya gharama kubwa ambapo mgonjwa mmoja huhitaji takriban Sh milioni 22.

Hata hivyo, Serikali imehakikisha wagonjwa wanaopatiwa matibabu hayo leo wanalipia kiasi kidogo, huku wasiokuwa na uwezo wakitibiwa bila malipo.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa moyo kutoka Hospitali ya Shifa nchini Misri, Prof. Mohamed Atef, amesema tiba hiyo inatoa matumaini makubwa kwa wagonjwa ambao shinikizo lao la damu limekuwa sugu licha ya kutumia dawa kwa muda mrefu.

“Leo tunatarajia kuwatibu wagonjwa sita hadi saba kwa upasuaji mdogo kupitia tundu dogo kwenye paja, ambapo tunaunguza mishipa inayopeleka damu kwenye figo,” amesema Prof. Atef.

Amesisitiza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika huduma za moyo na kuitaja JKCI kama taasisi ya mfano barani Afrika kutokana na huduma zake za kibingwa na jitihada za kuendeleza teknolojia mpya za matibabu.

“Ninafuraha kuwa daktari wa kwanza kufikisha teknolojia hii JKCI. Naupongenza uongozi kwa kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma za kisasa na mbinu mpya za tiba,” ameongeza Prof. Atef.

Mmoja wa wagonjwa wanaopatiwa huduma hiyo, Donasian Meleki, ameishukuru Serikali na JKCI kwa kumpunguzia gharama za matibabu.

Meleki amesema amekuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu tangu mwaka 2011 hali iliyomsababishia kupata matatizo ya figo na kuhitaji dialysis.

“Ninaishukuru Serikali kwa kujali afya za wananchi. Naamini matibabu haya yatanisaidia kurejea katika hali yangu ya kawaida na kuendelea kulitumikia Taifa,” amesema Meleki.

Tiba ya Renal Denervation ilianza kutolewa duniani mwaka 2013, lakini ilisitishwa kutokana na kutokuwepo kwa mafanikio ya kuridhisha.

Baada ya utafiti wa kina kufanyika, matokeo mapya yameonesha ufanisi mkubwa, na hivyo tiba hiyo kurejeshwa kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu sugu lisiloshuka kwa dawa.

Habari Zifananazo

6 Comments

    1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
      .
      Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  1. More than 720 000 people die due to suicide every year. Suicide is the third leading cause of death among 15–29-year-olds.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button