Joel Matip astaafu kandanda rasmi

BEKI wa zamani wa Liverpool, Joel Matip ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 33.

Beki huyo alijiunga na The Reds mwaka 2016 akitokea Schalke ya Ujerumani na kufanikiwa kuichezea Liverpool mechi 201, na kushinda mataji matano makubwa.

Matip alitoa pasi ya mabao katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2019 kwa bao la Divock Origi katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham mjini Madrid, na kuisaidia Liverpool kushinda Kombe lao la sita la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Advertisement

SOMA: Arsenal yawania saini za wawili Bournemouth

Majeraha yalimfanya mlinzi huyo afikishe mechi tisa pekee katika kikosi kilichoshinda Ligi Kuu ya England 2019-20, ambacho kilimaliza miaka 30 kusubiri taji la ligi.