Jokate Rais wa Kanda ya Afrika

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo ameteuliwa kuwa Rais wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Jukwaa la Viongozi Wanawake Afrika Africa Women’s Movement-AWM).

Jokate atakuwa na jukumu kuhakikisha Ukanda wa Afrika Mashariki unaendelea kupika na kutengeneza viongozi wanawake wengi zaidi katika kuchangia maendeleo endelevu na ustawi wa mataifa.

Pia, ameteuliwa kuwa mmoja kati ya vijana wachache mahiri watakaowakilisha ndani ya Mtandao wa Kimataifa wa Vijana unaochagiza maamuzi makubwa ulioko chini ya Club de Madrid.

Club de Madrid ni jukwa kubwa duniani linalounganisha pamoja Marais na Mawaziri Wakuu Wastaafu pamoja na Viongozi wengine mashuhuri kutoka kona zote za Dunia na kutumia uzoefu wao mkubwa ndani ya uongozi kustawisha demokrasia na ustawi wa Watu na maendeleo kiujumla.

Club de Madrid ni chombo cha kimataifa kisichofungamana kisiasa wala kisichotengeneza faida, chombo hichi kinatumia uzoefu na ushawishi mkubwa wa Wanachama wake wasiopungua 100 kutoka nchi zaidi ya 70 kushawishi maboresho endelevu ya sera na kupata Uongozi makini na mahiri katika kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa.

Akizungumzia uteuzi huo Jokate amesema “ninayo heshma kubwa kuchaguliwa mwanajumuiya wa Mtandao wa Vijana mahiri chini ya Club de Madrid.

Mtandao huu mkubwa Duniani unatoa nafasi kwa viongozi vijana kama mimi kukutana pamoja, kujifunza na kuchagiza maendelezo endelevu.

Nina shauku kubwa na kesho ya vijana wenzangu.

”Amesema

Amesema nifuraha kwake kukutana na vijana mahiri ambao ni sehemu ya Mtandao wa Vijana wenye ushawishi katika maamuzi. Vijana hao wanaleta mabadiliko chanya Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na Kanda ya Karibea(Caribbean), na wote kwa pamoja wanachochea kasi ya maendeleo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button