TIMU ya Namungo imemtangaza Juma Mgunda kuwa Kocha Mkuu mpya wa klabu hiyo.
Taarifa ya Namungo imesema Aliyekuwa Kocha Mkuu Mnwinyi Zahera amebadilishwa majukumu sasa atakuwa mshauri wa benchi la ufundi.
SOMA: Namungo na Kitambi ndio basi tena
“Uongozi wa Klabu ya Namungo unapenda kuujulisha umma kuwa umefikia makubaliano na Kocha Juma Rmadhani Mgunda kuwa Kocha Mkuu wa klabu yetu, akisaidiwa na Kocha Ngawina Ngawina, Shadrack Nsajigwa na Vladimir Niyonkuru,” imesema taarifa hiyo.
Kumekuwa na wimbi la makocha wa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara kutimuliwa kazi tangu kuanza msimu mpya wa 2024/2025 kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hizo.
Namungo ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 7.