Kaa wanaoangua nazi hatarini kutoweka

DAR ES SALAAM;  Samaki kaa wajulikanao kama ‘tuyuli’ wapo hatarini kutoweka kutokana na kuonekana kwa uchache katika maeneo ya ukanda wa Pwani.

Ofisa Habari wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Ivan Kimaro amesema hayo alipozungumza na HabariLEO Digital na kueleza kuwa sifa kubwa ya samaki hao ni wakubwa na wana uwezo wa kupanda mti wa mnazi na kuangua nazi, kuishusha chini kuifua na kuila.

Advertisement

Soma: Watafiti waja na chanzo ugonjwa wa kuvilia damu samaki

Amesema anafanya hivyo kwa kuwa nazi ni chakula chake kikubwa, anatumia meno ya mbele kuvunja nazi hiyo kuipasua na kuila.

Vile vile tuyuli ana uwezo wa kuishi mpaka miaka 60, pia kuwa na uzito kilo nne.

Kwa Dar es Salaam wanapatikana visiwa vya Bongoyo na Mbudya, ambavyo wanavihifadhi kuhakikisha rasilimali hiyo inaendelea kuwepo kwa kuwa aina hiyo inakaribia kutoweka.