Kagis yaongezewa uwekezaji kukomesha ukatili Geita

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Rafiki Social Development Organisation (RAFIKI SDO) limetenga zaidi ya Sh milioni 30 kwa mwaka huu wa fedha kufanikisha kampeni ya kupinga ukatili na Kusaidia Wasichana Barehe Kuendelea na Masomo (KAGIS).

Mashindano hayo yanaendeshwa katika mikoa ya Geita na Kigoma chini ya waratibu wa Mradi wa KAGIS unaotelezwa na Shirika la RAFIKI- SDO kwa ushirikiano na shirika la Plan International na kufadhiliwa na serikali ya watu wa Canada.

Meneja Mradi wa KAGIS kutoka Rafiki SDO, Eliud Mtalemwa amesema hayo katika mahojiano maalum na HabariLeo amesema kupitia mashindano wanatoa ujumbe wa kuhamasisha jamii kuachana na mila kandamizi na ukatili wa kijinsia.

Advertisement

Amesema matumizi ya michezo kuhamasisha kampeni ya KAGIS imeonyesha tija kwani mwitikio wa vijana hususani vijana barehe wa jinsia zote ni mkubwa ikilinganishwa na mikutano ya hadhara ambayo mara nyingi mwitikio unakuwa mdogo.

“Kumekuwa namatokeo chanya mashindano haya yamekuwa chachu ya mabadiliko tulipoanza mwaka 2021 hali haikuwa hivi sasa ivi mwamko ni mkubwa vijana wanakuja na wanapokea ujumbe na wao wenywe wamekuwa wahamasishaji.”

Amesema kupitia michezo waratibu wa mradi wa KAGIS wanapata fursa ya kutoa elimu kwa jamii juu ya afya ya uzazi na hedhi salama pamoja na kuhamasisha suala la usawa wa kijinsia kwa kumwezesha mtoto wa kike kupata elimu na fursa tofauti..

Ofisa Mtendaji kata ya Kasamwa mjini Geita ambapo yanafanyika mashindano hayo, Victor Bashingwa amekiri mradi wa Kagis umesaidia kudhibiti utoro shuleni na ukatili hasa kwa wanawake na watoto na kutoa uelewa wa pamoja kwa jamii kupitia michezo.

Amesema kabla ya mradi kufika kwenye kata hiyo utoro kwa wanafunzi ulikua mkubwa hasa siku za mnada ambazo watoto wa kike walitumika kufanya kazi ya kuosha vyombo kwenye migahawa au kuuza bidhaa mnadani badala ya kwenda shule.

Ofisa elimu kata ya Buhalahala, Amos Nyamsika amesema kabla ya mradi huo changamoto ya utoro na ukatili kwa mtoto wa kike ilikuw akubw alakini sasa mabadiliko yanaonekana baada ya mahudhurio shuleni kuongezeka.

“Utoro kwa mtoto wa kike ulitokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukosa taulo za kike lakini mradi huu umekuja na elimu ya kushona sodo lakini pia wanagawa taulo za kike mashuleni hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa.” Ameeleza

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *