Kais Saied kushinda tena urais

TUNISIA : RAIS wa Tunisia Kais Saied anatarajiwa kushinda uchaguzi wa urais nchini humo kwa asilimia 89.2 ya kura licha ya idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa katika vyombo vya habari nchini humo, Saied mwenye umri wa miaka 66, anatarajiwa kupata ushindi wa kishindo na kuwabwaga wapinzani wake  Ayachi Zammel ambaye yuko gerezani na Zouhair Maghzaoui.

Makundi ya wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini humo wanamtazama Rais  Kais Saied ni mtu mwenye a madaraka na sio mwenye kufuata misingi ya kidemokrasia.

Advertisement

SOMA : Mgombea urais atupwa jela Tunisia

Tume ya uchaguzi ISIE imefahamisha kuwa takriban watu milioni 9.7 walikuwa na haki ya kupiga kura katika nchi hiyo yenye idadi jumla ya watu milioni 12.