Mgombea urais atupwa jela Tunisia

TUNISIA : MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya upinzani nchini Tunisia,Ayachi Zammel amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela baada ya kutiwa hatiani kwenye mashitaka manne, likiwemo la kughushi kura zilizomuidhinisha kuwa mgombea wa urais.

Wakili wa Ayachi Zammel, amesema licha ya hukumu hiyo kutolewa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini humo Zammel ataendelea kubakia kama  mgombea katika uchaguzi huo wa rais unaotarajia kufanyika Oktoba 6, mwaka huu.

Zammel ambaye ni mbunge wa zamani na mfanyabiashara anaongoza chama kidogo cha kiliberali na amekuwa ni mmoja kati ya wagombea wawili walioidhinishwa na Tume ya Uchaguzi ya Tunisia kupambana na Rais Kais Saed katika uchaguzi huo wa rais.

SOMA: Rais mstaafu Tunisia jela miaka minane

Hatahivyo,Tume ya uchaguzi nchini humo pia  imewazuia wagombea wengine 14 kuwania kwenye uchaguzi huo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button