Kajuna kucheza robo fainali mabingwa mikoa

TIMU ya soka ya Kajuna FC ya Mkoa Kigoma imejihakikishia kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya mikoa kwa kufikisha pointi 13.

Pointi hizo zinaifanya timu hiyo kujihakikishia kuwa moja ya timu mbili zitakazocheza hatua hiyo kutoka Kituo cha Kigoma.

Matumaini hayo yanakuja baada ya timu hiyo kufikisha poiti 13 baada ya kubanwa na kutoka suluhu katika mchezo wake wa tano kati ya michezo sita wanayopaswa kucheza ambapo ni timu ya Igunga ya Tabora inayoweza kufikisha pointi hizo ambapo kwa sasa ikiwa na pointi 10 na michezo miwili mkononi.

Katika mchezo wake wa tano dhidi ya timu ya Dew Drop ya Mkoa Sumbawanga uliofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma timu ya Kajuna ilishindwa kupata ushindi na hivyo kutoka suluhu ya bila kufungana na hivyo kutia doa ushindi mfululizo wa mechi zake nne ilizocheza awali.

Kwa sasa kwa matokeo hayo Kajuna inaongoza kituo hicho baada ya kukusanya pointi 13 ikibakisha mchezo mmoja ikifuatiwa na timu ya Igunga ya Tabora yenye point 10 iliyobakisha michezo miwili huku timu ya Home Boys ya Katavi ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na point saba ikiwa imecheza michezo mitano hivyo iwapo itashinda mchezo wake wa mwisho inaweza kufikisha point 10 ambazo tayari timu zinazoongoza zimeshazifiki

Timu ya kyela FC ya Mbeya inashika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi sita baada ya kucheza michezo minne ikiwa imefungana pointi naa Timu ya The Green ya Songwe ambayo pia ina pointi sita huku timu ya Dew Drop ya Sumbawanga mkoani Rukwa ikiwa na point moja na timu ya Magic Pressure ya Singida ikiwa haina pointi baada ya kucheza michezo minne.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button