Kamati Kuu ACT yakutana leo
KAMATI Kuu ya Chama cha ACT wazalendo imekutana leo Agosti 24, kujadili Agenda mbalimbali ikiwemo kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman kilifanyika makao makuu ya chama Magomeni, Dar es Salaam.
SOMA: ACT kujadili uchaguzi mitaa
Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mwenezi wa chama hicho, Shangwe Ayo imeeleza kuwa Agenda iliyojadiliwa ni pamoja na kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.
“Ufunguaji wa kesi kupinga Tamisemi kusimamia uchaguzi serikali za mitaa,” imeeleza taarifa hiyo.