DAR ES SALAAM: KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imeeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB).
Kauli hii inakuja wakati benki hiyo ikiendelea kutoa gawio kwa serikali kuu na kuiwezesha kutekeleza miradi ya kimkakati.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo, Augustino Vuma mwishoni mwa juma wakati kamati hiyo ilipotembelea benki hiyo ili kufahamu mikakati, utendaji kazi pamoja na mwelekeo wake kwa mwaka 2025.
Amesema pamoja na mambo mengine ushirikiano wa benki hiyo na taasisi nyingine za serikali ikiwemo Shirika la Reli Tanzania -TRC, katika utoaji wa huduma imetajwa kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Adam Mihayo amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na kijamii na kiuchumi.
SOMA: TCB yatoa mikopo ya Sh trilioni 1.1 kuwezesha wajasiriamali
Itakumbukwa kuwa Kamati hiyo imekua ikifanya ziara yake ya kutembelea taasisi mbalimbali za Serikali ili kusikiliza changamoto zao, kuona utendaji wao wa kazi na kuwasilisha ripoti kwa serikali kuu.