Kambi ya usalama yashambuliwa Mali

MALI : Kambi ya Usalama huko Bamako katika mji mkuu nchini Mali imeshambuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari zimesema milio hiyo ya risasi imesikika  majira ya saa 5.30 asubuhi na kusababisha moshi mkubwa kutapakaa katika eneo hilo la usalama.

Hatahivyo shambulio hilo limefanywa katika kambi zaidi ya moja katika mji mkuu wa Mali.

Mali ni miongoni mwa nchi za Afrika Magharibi ambazo zimekuwa katika mapambano na waasi wa Kiislamu kwa zaidi ya muongo mmoja sasa na haijulikani ni nani aliyehusika na ufyatuliaji huo wa risasi .

Mnamo mwaka 2021, Jeshi liliamua kufanya mapinduzi na kuishutumu serikali kwa kushindwa kupambana na waasi hao.

SOMA: Ufaransa kuondoa ubalozi, wanajeshi Niger

 

Habari Zifananazo

Back to top button