Kampuni 27 Ufaransa kuwekeza Tanzania

Waona fursa kwenye teknolojia za miundombinu, nishati, usafirishaji na Maendeleo ya miji.

DAR ES SALAAM: UJUMBE wa wafanyabiashara kutoka kampuni 27 za Ufaransa upo nchini kwaajili ya kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji.

Wafanyabiashara hao wanajadili namna ya kuwekeza Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo, teknolojia za miundombinu, nishati, usafirishaji na Maendeleo ya miji.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano huo na kuongeza kuwa  mkutano huo ni muendelezo wa majadiliano yaliyofanywa na wafanyabiashara hao na Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea nchini huko Mei 2024.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe

Aidha ujumbe huo pia umesaini mikataba wa utunzaji wa mazingira pamoja na bayoanuai za misitu baina yao na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

SOMA: Kigahe: njooni muwekeze fursa zipo

Amesema ziko fursa kubwa za masoko nchini Ufaransa kwa bidhaa za kahawa,samaki za aina mbalimbali na hata mbegu za mbogamboga na kuwataka wananchi kuchangamkia eneo hilo.

Kigahe amesema serikali iko tayari kukaribisha wawekezaji kutoka Ufaransa  jambo litakalokuza uchumi wa Tanzania .

“Licha ya uwekezaji huo nchini lakini kuna fursa za masoko kwa bidhaa za Tanzania jambo linaloongeza wigo wa kuuza kwa wingi nchini humo,” amesema.

Amesema Kwa mujibu wa takwimu za Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ufaransa imewekeza Tanzania katika miradi 41 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 104.34 ambayo imetoa ajira 2379.

Amesema kampuni za Ufaransa zilizowekeza Tanzania ni katika maneno ya kilimo, ujenzi, usafirishaji, huduma,taasisi ,a fedha pamoja na rasilimali watu.

Amesema kupitia ujumbe huo wataona namna ya kushirikiana  kuboresha kilimo katika kuongeza thamani  katika mazao lakini pia kuongeza wigo wa kuuza bidhaa nchini Ufaransa.

Amesema Tanzania inapeleka bidhaa  Ufaransa zinazofikia Dola za Marekani milioni 25122 Kwa mwaka huku Ufaransa ikiingiza bidhaa zenye gharama ya Dola milioni 75.418 Kwa mwaka.

“Tunauza kidogo,t una kazi kubwa ya kuongeza uuzaji Ili kutanua wigo, hivyo wao watasbirkiana nao kupata teknolojia mpya za kisasa viwanda kutoka Ufaransa,” amesema.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchi Tanzania Nabil Hailaouit amesema Tanzania ni mojawapo ya nchini zenye utawala Bora na kuwa naazingira Bora ya uwekezaji.

Amesema uwekezaji Kwa wafaransa sio wa muda na kuondoka Bali ni endelevu wenye tija na manufaa kwa nchi zote.

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Ali Mwadini amesema Tanzania ni mojawapo ya nchi yenye miundombinu imara na inayounganisha mipaka mbalimbali.

Amesema Tanzania pia ina rasilimalibalbali zinazohitaji uendelevu kwa kizazi kijacho lakini pia kuma sera nzuri za uwekezaji.

Habari Zifananazo

Back to top button