Kampuni ya madini yawakumbuka waathirika mafuriko Simanjiro

KAMPUNI ya Franone Mining and Games inayojishughulisha na uchimbaji madini ya Tanzanite imeungana na Serikali kuchangia mahitaji mbalimbali ya chakula na vifaa kwa wahanga wa mafuriko wilayani Simanjiro mkoani Manyara vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 31 .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 10, meneja mkuu wa kampuni hiyo, Vitus Ndakize alisema kuwa wameguswa na tukio hilo hivyo kama watanzania waliowekeza kwenye uchimbaji wa madini na wao wameona wachangie Watanzania wenzao ambao wamepatwa na majanga hayo kwa kutoa bidhaa mbalimbali.

Alisema miongoni mwa vitu ambavyo wamechangia na kukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Seleman Selela ni magunia 200 ya mahindi , maharage gunia 40 ,sukari mifuko 20, na mafuta kantoni 40 za Lita moja moja ambayo imegharimu fedha za kitanzania Sh milioni 31.

” Kama Kampuni tumetoa kwa ujumla ila wao ndio wanajua namna watakavyogawanya  chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo husika “Amesema Vitus

Pia Vitusi amewashauri wadau mbalimbali kuendelea kujitoa nakwamba wakati mwingine majanga kama hayo yanapotokea watu wanakuwa hawajajipanga hivyo nivema kujitoa katika kile kidogo unachokuwa nacho na wao kama wawekezaji wamejitoa baada ya kuguswa kutokana na kile kimejitokeza

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo Simanjiro Christopher Ole Sendeka ameipongeza kampuni ya Franone kwa kuwachangia wahanga wa mafuriko hayo.

Sendeka amesema kampuni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwenye jamii kwani hivi karibuni wakati wa ukame ilisaidia chakula kwenye shule mbili zilizokuwa zinakabiliwa na uhaba wa chakula zilizopo kata ya Naisinyai

Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Asia Ngaliwason ameishukuru kampuni Franone na kuwahakikishia kwamba msaada huo utafika kwa wahusika waliokumbwa na mafuriko

Asia ameongeza kuwa waliokumbwa na mafuriko ni watu 126 na watapata msaada huo katika kata za shambarai na kata ya msitu wa Tembo kwenye kaya 49n

Habari Zifananazo

Back to top button