‘Karibu hapa ni nyumbani’

DAR ES SALAAM: Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imemkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji mpya, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi, ambaye ameingia kwenye nafasi baada ya kustaafu kwa Mkurugenzi wa awali, CPA Pius Maneno.

Prof. Sylvia Temu, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha Prof. Mzenzi, amesema kuwa bodi na menejimenti nzima wanafuraha kumpokea na kuendelea kushirikiana naye kwa ajili ya kuendeleza kazi za bodi katika kukuza na kusimamia tasnia ya uhasibu nchini.

“Leo, kwa niaba ya bodi na menejimenti yote ya NBAA, tunamkaribisha Mkurugenzi Mtendaji ambaye anachukua wadhifa huu baada ya kustaafu kwa Mkurugenzi wetu wa awali. Tutampa ushirikiano wa dhati na kufanya naye kazi kwa uelewa na uaminifu ili kuendeleza jukumu la bodi la kusimamia na kukuza tasnia ya uhasibu,” amesema Prof. Temu.

Prof. Temu pia amesema kuwa Prof. Mzenzi amejitahidi kutoa ahadi ya kushirikiana na wadau wote wa fani ya uhasibu na ukaguzi, ikiwemo wahasibu, wakaguzi wa hesabu, kampuni za ukaguzi, serikali, na washirika wa maendeleo.

Kwa upande wake, Prof. Mzenzi amesema kuwa atahakikisha ushirikiano na wadau wote wa ndani na nje ya Tanzania, na kuendeleza ubora wa fani ya uhasibu na ukaguzi kwa maendeleo ya taifa.

“Tutashirikiana na serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa fani yetu inakua na kufikia viwango vya kimataifa, na pia kuimarisha uwazi na mawasiliano na wananchi kuhusu shughuli zetu,” amesema Prof. Mzenzi.

NBAA ni bodi ya kisheria inayohusika na kusimamia na kukuza tasnia ya uhasibu na ukaguzi nchini Tanzania, ikihakikisha kufuata viwango vya kitaaluma, maadili, na uwazi katika kila kazi ya kitaalamu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button